Wednesday, 10 August 2016



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameanza ziara yake mkoani Mwanza ambapo amehutubia mamia ya wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza.









3














Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa siku 14 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI) Dkt. Othman Kiloloma kukaa na bodi ya taasisi hiyo kushughulikia matatizo ya watumishi ili kuleta ufanisi mzuri katika kitengo hiko.
Akizungumza na watumishi wa MOI Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemtaka Dkt. Kiloloma kukaa na bodi ya taasisi hiyo ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya watumishi wake ndani ya siku 14 ili wafanyakazi waweze kutoa huduma bora kwa watanzania.
“Naagiza Bodi ya MOI pamoja na Kaimu Mkurugenzi wake ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya watumishi wake ndani ya siku 14 ili kuondoa malalamiko na kuleta ufanisi bora katika taasisi hii”alisisitiza Mhe. Ummy.
Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa amepokea changamoto zao na za taasisi hyo nakuhaidi kuzitatua ndani ya mwezi mmoja na kuwataka wasichoke kutoa huduma bora kwa watanzania ili kuokoa maisha yao na kupambana na umaskini.
Mbali na hayo Mhe. Ummy ameagiza watendaji wa Wizara yake kuleta mkakati wa kupambana na kupunguza ajari za barabarani hasa zitokanazo na bodaboda ndani ya siku 14 ili kuwapa nafuu madaktari na wauguzi wa MOI kuweza kuondoa mlundikano wa wagonjwa hospitalini hapo.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi MOI Dkt.Othman Kiloloma amesema kuwa mbali na changamoto wanazokutana nazo wamefanikiwa kuunda upya wafanyakazi wataoweza kufanya upasuaji kwa wagonjwa wa jumamosi na itaanza mara moja.
Aidha Dkt. Kiloloma ameongeza kuwa MOI imeweza kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 1.1 kwa mwezi kutoka kiasi cha shilingi milioni 400 kwa kipindi kilichopita.






Nimewasili mkoa wa Katavi,nimefanya ukaguzi kwenye kambi ya wakimbizi ya KATUMBA ambako kuna zoezi la uhakiki wa waliokuwa wakimbizi kutokea kwa majirani zetu Burundi na baadae tuliamua kuwapa uraia wa Tanzania mwaka 2009.
Zoezi hili la uhakiki linafanyika ilikuchunguza mienendo yao na uwepo wao kwenye eneo la kambi.Kumekuwepo nataarifa za baadhi ya ndugu zetu hawa kujihusisha na watu waovu,kufanya vitendo vya kibaguzi na kutoka nje ya kambi zao na kwenda nchi jirani bila kibali.
Mbali na kambi ya katumba,pia nimetembelea kambi ya Mishamo.Nimewaagiza vyombo vya usalama na kupitia serikali za mitaa kuwachukulia hatua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Tanzania hatua tabia za kibaguzi,moja kati ya sifa kubwa ya nchi yetu ni kushinda vita dhidi ya ubaguzi wa aina yoyote tangu tulipopata uhuru.
Natoa rai kwa raia wote tuliowapa kibali cha kufanya kazi,kuishi na kuwa raia wa nchi yetu, waache kujihusisha na vitendo viovu na vyakibaguzi.Hatutawavumilia watu ambao tumewakaribisha kwa nia njema hapa nchini na baadae wahatarishe usalama na amani ya nchi yetu.
Vilevile nimekutana na askari wetu wa jeshi la polisi na idara zake zote na nimetembelea gereza la mpanda ikiwa ni ziara ya kupata uhalisia wa changamoto zinazokabili jeshi la polisi,magereza,uhamiaji na zimamoto kwa kila mkoa,tayari kwa majawabu ya kudumu.
"usalama wetu,jukumu letu sote"


























Tuesday, 9 August 2016


Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015 tulieleza malengo yetu kwa wananchi. Leo tunatoa mrejesho wa utekelezaji kama tulivyoahidi. Ifahamike kuwa huu ni mwaka wa kwanza wa Bajeti hivyo mambo mengi ni ' work in progress '. Bado kuna changamoto nyingi sana ikiwemo kuhakikisha kuwa Mpango kabambe wa mji wetu unakamilika na kutekelezwa.
1. Kushirikiana na Wabunge wa Mkoa wa Kigoma kuhakikisha barabara zote za mkoa zinaunganishwa Kwa Lami. Barabara za Kigoma - Nyakanazi, Mwandiga - Kagunga na Simbo - Kalya ni mfano wa barabara hizo. ------ UTEKELEZAJI: katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17 tumefanikiwa kupata Mradi wa barabara ya Manyovu - Kasulu - Kibondo jumla ya kilometa 240. Benki ya Maendeleo ya Afrika itafadhili barabara hii na TANROADS itaigawa kwa kuweka wakandarasi 4 ili ikamilike kabla ya mwaka 2020. Barabara ya Mwandiga - Kagunga TANROADS Mkoa imeshatangaza zabuni za kuanza kuifungua na mchakato wa kupata mkandarasi umeanza. Pia Barabara ya Msimba - Ujiji ( Kasulu Road ) inajengwa Kwa Lami na kilometa nyengine 10 ikiwemo ya Mwembetogwa - Msikitini Kigoma zinajengwa Kwa Lami. Zabuni ya kujenga mzunguko ( roundabout ) ya Mwanga Sokoni tayari imetangazwa na kufunguliwa na ujenzi unaanza mwaka huu wa Fedha 2016/17.
2. Kuhakikisha kuwa Mitaa ya Manispaa inakuwa na miradi maalumu ya kujengwa mifereji na barabara za Lami na mawe Kwa lengo la kusafisha mji na kuzalisha ajira Kwa vijana. Pia kumaliza kero za miundombinu Mto Luiche kata ya Kagera [ kwa kujenga daraja na barabara kutokea Ujiji ]. ----UTEKELEZAJI: Mkandarasi wa kujenga mfereji wa Lubengela ameanza Kazi ya kukusanya vifaa ( mobilization ). Mtaa wa Rusimbi Ujiji na Barabara ya Shindika - Jihad - Katubuka na Barabara ya Mwami Rusimbi Gungu ipo kwenye Mpango wa kuwekwa Lami. Mradi wa kuweka Lami Mitaa ya MwembeNgoma - Kisangani - Msufini - Kwa Bella na barabara ya Kaya - Simu zinajengwa kwa lami. Manispaa imekubaliana kimsingi na Shirika la BTC la Ubelgiji kufanya upembuzi yakinifu na Usanifu wa kina wa Mitaa ya Mawe/pavements katika kata 8 za Manispaa. Barabara ya Ujiji - Kagera ikiwemo Daraja la Mto Luiche ni sehemu ya Mradi mkubwa wa Umwagiliaji katika Mto Luiche. Usanifu wa Barabara ya ufukweni kutoka Forodha ya Ujiji mpaka Katonga ( Kikamba ( Bangwe) - Ujiji Forodhani road ( planned) unafanyika mwaka 2016/17 na Barabara ya Bangwe - Ujiji ipo kwenye Mpango wa TANROADS. Mtaa wa Mzee Menge unawekewa ' pavement ' wote Kwa ajili ya Soko la Jioni ( Mzee Menge Street Night Market Project ). Barabara ya Msimba - Ujiji ( Kasulu road ) tumeiorodhesha kwenye miradi ya Barabara za ahadi za Rais za 10km za Lami katika mji wetu.
3. Kuboresha mazingira ya Biashara Kwa kuondoa kero ya ushuru Kwa wafanyabiashara wadogo Kwa mujibu wa Sheria ndogo za Manispaa, kuboresha Bandari zote na kujenga Bandari mpya(jetty) eneo la Forodha ya Ujiji ili kurudisha hadhi ya mji wa Ujiji. ------- UTEKELEZAJI: Mamlaka ya Bandari ( TPA ) inatangaza zabuni ya ujenzi wa Jetty Forodha ya Ujiji Mwezi Agosti 2016, pia Bandari ya Kibirizi. Sheria ndogo tunazopendekeza Kwa Waziri wa TAMISEMI zinarekebisha kodi na tozo Kwa kufuta kabisa ushuru wa wanaotandika bidhaa chini. Soko jipya la Jioni Mtaa wa Mzee Menge linaanzishwa kutoa fursa ya Wafanyabiashara wadogo kufanya biashara bila bugudha. Shirika la PSPF linaanza ujenzi wa Soko la Mwanga ambapo ndani yake kutakuwa na Mnada wa Kimataifa wa Asali. Baada ya Soko la Mwanga kukamilika, Soko la Mjini Kigoma litabolewa na kujengwa Shopping Mall. Soko la Ujiji lina Mradi maalumu wa kujenga Kituo cha Kikanda cha Biashara ( trading and logistical center - Ujiji City Project ). Mradi huu utakaotokana na uwekezaji kutoka nchini China utawezesha ujenzi wa maduka 3000, Warehouses na nyumba za makazi. Lengo la Mradi huu ni kuwezesha Ujiji kuwa eneo ( a Hub ) la wananuzi wa bidhaa kutoka Nchi za Maziwa Makuu badala ya watu hao kusafiri kwenda Mashariki ya mbali. Kupitia Miradi ya LIC inayofadhiliwa na Serikali ya Denmark, Manispaa inatarajia kuweka mazingira bora ya biashara Kwa kuondoa vikwazo ili Wafanyabiashara waweze kuwekeza, kufanya biashara na kuzalisha ajira nyingi Kwa wananchi. Manispaa pia inatengeneza ' masterplan ya mji ' ili kuupanga vema. Katika mipango ya muda Mfupi Manispaa imeanza mchakato wa kuomba kuongeza eneo lake ili kukidhi haja ya ongezeko la watu na shughuli za uchumi. Manispaa imeomba kuongeza kata za Mwandiga, Simbo, Msimba na Ziwani zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Kigoma ili ziingizwe Manispaa.
4. Kuhamasisha vikundi vya Wananchi kama wavuvi, kina mama, wakulima wa bustani, waendesha vyombo vya usafiri na kuviunganisha na mifuko ya hifadhi ya jamii Kwa kuchangia sehemu ya michango yao ili wapate mafao ya kama mikopo nafuu na Bima ya afya. 50% ya Bajeti ya Mfuko wa Mbunge itachangia Mfumo wa Hifadhi ya Jamii wa Manispaa. ----UTEKELEZAJI: Baraza la Madiwani limepitisha Skimu ya Hifadhi ya Jamii ya Manispaa Kwa ajili ya utekelezaji. Mwaka 2016/17 Fedha za Mfuko wa Mbunge zimesaidia kuondoa changamoto ya madawati. Fedha zitokanazo na 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri zitatumika kuchangia vikundi vya Vijana na Wanawake kwenye Hifadhi ya Jamii na kuwawezesha kupata Mikopo. Manispaa imefanya mazungumzo na Benki ya Dunia ili wachangie katika Skimu hii Kwa lengo la kuhakikisha wananchi wote wa Manispaa wanakuwa na Bima ya Afya. Manispaa bado inaendelea kufanya mazungumzo na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili kupata Mfuko mwafaka wa Kuendesha Skimu hii. Skimu hii, pamoja na mambo mengine, itaongeza uwezo wetu wa kuweka Akiba Kwa ajili ya uwekezaji wa ndani ili kukuza uwezo wetu wa uzalishaji ( productive capacity ).
5. Kushirikiana na Wabunge wa Mkoa wa Kigoma kuanzisha Benki ya Kigoma ili kuwezesha Wafanyabiashara wa Kigoma kukuza mitaji yao na hivyo kupanua [ Biashara ] zao. ----UTEKELEZAJI: bado hatujachukua hatua zozote. Baada ya Skimu ya Hifadhi ya Jamii kuanza rasmi Manispaa ya Kigoma itaweza kuanzisha Benki ya Jamii ( community Bank ) na kualika Halmashauri nyengine mkoani na Vyama vya Ushirika kuwa wanahisa na hivyo kutimiza malengo yetu.
6. Kusimamia kikamilifu kuanza Kwa Mradi wa kufua umeme Kwa kutumia maporomoko ya maji katika Mto Malagarasi ( Igamba III ) na kumaliza kabisa tatizo la umeme wa uhakika mkoani Kigoma. ------ UTEKELEZAJI: Bajeti ya mwaka 2016/17 imetenga Fedha Kwa ajili ya kuanza kutekelezwa Kwa ujenzi wa kituo cha kufua umeme cha Igamba III ( Malagarasi Hydro Power ). Hata hivyo Manispaa inafanya mazungumzo na wadau mbalimbali wa Maendeleo ili kuweza kuwa na Mradi mkubwa wa Umeme mbadala Kwa ajili ya kuendesha mitambo ya Maji na kuwezesha kila nyumba kuwa na umeme. Mipango hii ikikamilika tutatoa Taarifa kwa wananchi.
7. Kuhakikisha Mradi mkubwa wa Mpunga katika Bonde la Mto Luiche unaanza ili kuzalisha ajira katika Kilimo na Viwanda vya Mazao ya kilimo. --- UTEKELEZAJI: Serikali ya Kuwait imekubali kufadhili Mradi huu wenye thamani ya US$ 15 milioni ikiwemo Miundombinu ya barabara na madaraja kuelekea kwenye Mradi.
8. Kumaliza tatizo la fidia Kwa waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma [ Gombe-Mahale International Airport ] na miradi ya Bandari Kavu Kibirizi na Katosho. ---- UTEKELEZAJI: zabuni ya ujenzi wa jengo la abiria ( passenger terminal ) na barabara za kuingia Uwanja wa Ndege wa Kigoma tayari zimeandaliwa na kupelekwa European Investment Bank Kwa ajili ya kupata kibali. Zabuni ya kuongeza Urefu wa Uwanja kufikia mita 3000 ili ndege kubwa ziweze kutua bado Kwa sababu ya changamoto ya fidia. Wananchi wanasema fidia ni ndogo. Changamoto hiyo pia ipo Kwa fidia za Bandari Kavu ya Katosho. Tunaendelea na juhudi ya kupata mwafaka ili miradi hii ianze kutekelezwa.
9. Kusimamia uanzishwaji wa Viwanda kupitia KiSEZ. Tutaanza na Viwanda vya mazao ya Mawese/Michikichi na viwanda vya kuchakata Samaki kufuatia kuboresha Uvuvi. ---- UTEKELEZAJI: miradi hii inategemea sana kumalizika Kwa tatizo la umeme. Hata hivyo chini ya miradi ya LIC inayofadhiliwa na Serikali ya Denmark, Mradi wa Uvuvi unaanza kuboreshwa na miradi ya uzalishaji wa Michikichi kupitia sekta binafsi. Manispaa pia imepitisha kanuni za mabwawa ya kufuga samaki ili kuwekeza kwenye mabwawa yaliyopo ndani ya Manispaa.
10. Kuendelea kuwatetea watu wa Kigoma dhidi ya unyanyasaji kuhusu uraia wao na kukomesha kabisa manyanyaso hayo Kwa kuhakikisha kuwa kipaombele cha vitambulisho vya uraia kinakuwa mji wa Kigoma. ---- UTEKELEZAJI: ni Kazi endelevu
11. Kuanzisha timu ya soka ya manispaa na kuhakikisha inafika ligi kuu. Hii litaenda na kuanzidhwa Kwa shule Maalumu ya Michezo (sports academy) ili kukuza vipaji vya Soka. ---- UTEKELEZAJI: hivi sasa kuna timu ya Kigoma ya Mvuvumwa FC ambayo ipo daraja la kwanza. Tunadhani ni vema kuiunga mkono timu hiyo ili kuiwezesha kupanda daraja kufika ligi kuu badala ya kuanzisha timu mpya. Manispaa ina mazungumzo na Klabu ya Azam Kwa ajili ya kufungua Tawi la Academy yake katika uwanja wa Kawawa, Ujiji. Manispaa pia inafanya mazungumzo na wafadhili kuanzisha Mwami Ruyagwa Youth Park ( MRYP) katika eneo la Mwanga Community Centre ili kutoa mafunzo ya Michezo mbalimbali Kwa vijana na kuibua vipaji.
12. Kukuza Utalii ili kuzalisha ajira Kwa vijana wengi zaidi wa mkoa wa Kigoma. ---- UTEKELEZAJI: Manispaa inajenga Tourist Information Centre katika eneo la Kigoma Mjini mbele ya Soko la Kigoma Kwa kushirikiana na TANAPA.
13. Kufuatilia kikamilifu na kumaliza kabisa changamoto ya wavuvi kuvamiwa na kuporwa Mali zao. UTEKELEZAJI: ni Kazi endelevu
14. Kukamilisha mradi mkubwa wa Maji ili kumaliza tatizo la maji; kupitia Hifadhi ya Jamii kuhakikisha kila mwananchi anapata matibabu; na kusimamia kikamilifu uboreshwaji wa elimu katika manispaa - kuboresha Chuo cha VETA, Kuanzisha High School 2 na kuboresha Shule za Msingi. ----- UTEKELEZAJI: Mradi wa Maji unakamilika na tunatarajia kuwa ifikapo Mwezi Oktoba Mradi wa Maji Kigoma utakuwa umekamilika. Hivi sasa mabomba yanatandazwa. Changamoto kubwa itakuwa ni gharama za nguvu ya umeme kuendesha mitambo hii. Tumeanza mazungumzo na wadau ili kuweka Solar Panels za kuzalisha umeme wa kutosha kuendesha mtambo na ziada kuuza TANESCO. Shule ya Buronge High School inaanza 2016/17 na itafuatiwa na Shule ya Kichanga Chui. Lengo letu ni kukamilisha High School 3 za Manispaa mpaka ifikapo mwaka 2019. Hata hivyo, tuna Mradi maalumu wa kuibadili Shule ya Msingi Kigoma ( Aghakan ) kuwa High School ya masomo ya Sayansi tu na kuhamisha Shule ya Msingi Kigoma kwenda eneo la jirani na makazi ya Mkuu wa Mkoa. Madawati ya Shule za Msingi na Sekondari yametengenezwa na mikakati mbalimbali ya kuboresha elimu inafanyika. Mwezi Septemba 2016 kutakuwa na Tamasha kubwa la kuchangisha zaidi ya tshs 300 milioni Kwa ajili ya kumaliza kabisa changamoto ya Madawati. Tamasha Hilo litaendeshwa na Mwanamuziki mkubwa nchini mwenye asili ya mkoa wa Kigoma. Tunafanya jitihada za kupata Ujiji Technical School yenye uwezo wa kudahili wanafunzi 5000. Upande wa Afya, Manispaa inatumia teknolojia Kudhibiti upoteaji wa dawa katika zahanati na vituo vya afya. Mfumo huu uliandaliwa na mvumbuji kijana mwenye asili ya Kigoma ndg. Bukhary Kibonajoro.
15. Kuanzisha na kuendesha Jukwaa la viongozi wa Dini ili kuendeleza mahusiano mema Kati ya waumini wa dini mbalimbali. --- UTEKELEZAJI: lilianza kutekelezwa tangu wakati wa kampeni. Kila mwaka Mara 2 tutakuwa tunakutana na Viongozi wa dini ili kujadili changamoto mbalimbali za mji wa Kigoma Ujiji.
Manispaa yetu bado inakabiliwa na Changamoto lukuki lakini kubwa kuliko yote ni changamoto ya uchumi - uzalishaji na ajira. Mzunguko wa Fedha kwenye mji bado ni mdogo sana kutokana na uzalishaji mdogo kwenye Kilimo na Uvuvi, kukosekana Kwa Viwanda hasa Viwanda vya kuongeza thamani ya Mazao ya Kilimo na Uvuvi na biashara ya Kimataifa kutochangamka licha ya Kigoma kuwa mpakani na Nchi nyengine na kuwepo Kwa Bandari ya Kigoma. Tusipokabiliana na changamoto hizi jitihada za kujenga Miundombinu hazitakuwa na maana sana. Mradi wa Ujiji City ( trade and logistical Hub ) utaweza kuongeza biashara ya Kimataifa na hivyo mzunguko wa Fedha. Vile vile Mradi wa Umwagiliaji Delta ya Mto Luiche utasaidia kukuza uzalishaji katika Kilimo na Viwanda vidogo. Kuna haja ya kuongeza juhudi katika Viwanda vya Mawese na Mazao yake kama sabuni nk na pia uzalishaji wa mbogamboga. Vile vile sekta ya Utalii inaweza kuwa chachu kubwa ya Maendeleo ya Manispaa.
Manispaa pia imejiunga na Mpango wa kuendesha Serikali Kwa uwazi ( OGP ) ili kuwezesha kuboresha utawala bora. Lengo la Manispaa ni kuweka mikataba yake yote wazi, kuweka wazi mchakato wa Bajeti ya Manispaa na kuendesha sekta za Elimu, Afya na Ardhi Kwa namna ambayo wananchi wanashiriki Kwa ukaribu mkubwa na kuwajibisha Viongozi.
Shabaha yetu ni kuwa Manispaa ya mfano nchini Tanzania.
Zitto Ruyagwa Zuberi Kabwe, Mb
Kigoma - Ujiji
9/8/2016


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenda kufanya ukaguzi maalumu katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya baada ya kuwepo kwa ubadhilifu katika ujenzi wa soko la Mwanjelwa.

“Inasikitisha ujenzi wa soko hili kuingia ubabaishaji. Ujenzi wa soko ungegharimu sh bilioni 16 ila sasa watendaji wamefanya mambo ya hovyo na kufikia sh bilioni 26 hatuwezi kuwavumilia lazima hatua zichukuliwe kwa wote watakaobainika katika ubadhilifu huu,” alisema.
 
Pia amempa siku tatu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla kufanya uchunguzi na kubaini nani aliyetafuna sh milioni 489 zilizotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya uendelezaji wa soko hilo ambazo hazijulikani zilipo.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo leo (Jumanne, Agosti 09, 2016) wakati alipofanya ziara ya kushitukiza katika soko la Mwanjelwa na kubaini ubadhilifu wa fedha katika ujenzi wa soko hilo.

Waziri Mkuu amesema mara baada ya CAG kumaliza kufanya ukaguzi atatoa taarifa na mtu yeyote atakayetajwa katika ripoti hiyo kuwa amehusika na ubadhilifu huo atawajibika hata kama yuko nje ya Jiji la Mbeya.

Alisema kitendo cha kuongeza gharama za ujenzi wa soko hilo kutokana na kuchelewa kwa ujenzi wake kinaisababishia Halmashauri yaJiji kulipa sh milioni 200 kila mwezi kwa ajili ya marejesho, hivyo aliagiza aliyesababisha gharama hizo asakwe na achukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amemtaka Mkuu wa Mkoa Mbeya, Amos Makalla kuhakikisha mtu aliyepangishwa katika kibanda cha kukusanyia uchafu sokoni hapo anaondolewa haraka na kurudishiwa fedha zake ili kibanda hicho kitumike kama ilivyokusudiwa.

Pia alimuagiza Mkuu huyo wa Mkoa kufanya ukaguzi katika vyumba vya maduka sokoni hapo na ifikapo Jumatatu mtu hajaweka mali anyang’anywe na kupangishwa kwa mtu mwingine mwenye kuhitaji.

Alisema hayo baada ya baadhi ya wafanyabiashara kulalamika kuwa kuna watu wamechukua vyumba vingi vya maduka kwa ajili ya kuvipangisha kwa wafanyabiashara kwa gharama kubwa tofauti na inayotozwa na Halmashauri, hivyo kunyima nafasi kwa walengwa kunufaika na soko hilo.

Mmoja wa wajasiriliamali sokoni hapo Mohammed Said alisema watu wameshika vyumba na kuviuza kwa sh milioni 20 hadi 40 kulingana na eneo kilipo chumba jambo linalosababisha baadhi ya wafanyabiashara kushindwa kupata nafasi katika soko hilo.

Awali Mkuu wa Mkoa alisema soko hilo linakabiliwa na matatizo mbalimbali kwani hata wahanga waliokuwa wanafanya biashara kabla ya soko kuungua moto hawakupewa kipaumbele wakati wa upangishaji wa vyumba vya maduka.

Kuhusu suala la kukosekana kwa wateja sokoni hapo Makalla amewataka wafanyabiashara wote wanaofanya shughuli zao katika maeneo yasiyokuwa rasmi kuhamia sokoni hapo mara moja.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, AGOSTI 08, 2016.



















































































































Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imevipiga faini ya Shilingi milioni kumi na tisa vituo viwili vya Televisheni na kimoja Cha Redio kutokana na kukiuka maadili na kanuni za huduma za utangazaji ya mwaka 2005.
Uamuzi wa kuvipiga faini vituo hivyo vya habari umetolewa na Kamati ya Muadhui baada ya kupitia mashauri matatu na kujiridhisha kuwa wamekiuka maadili.
Kituo cha utangazaji cha ITV kimepigwa faini ya shilingi milioni kumi kutokana na makosa mawili ambapo kosa mojawapo ni kipindi cha KUMEKUCHA kutumika kumkashifu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Tulia Akson.
Clouds Radio nao wamepewa onyo la kukiuka kanuni za huduma za utangazaji na kutozwa faini ya shilingi milioni 5 kutokana na Watangazaji wa kipindi cha JAHAZI kusikika wakishabikia taarifa ya ufanyaji ngono kati ya mtu na mbuzi.
Adhabu ya aina hiyo imewakumba pia wenzao wa Clouds Tv ambao wamepigwa faini ya shilingi milioni tano kwa kurusha hewani video za wimbo THANKS FOR COMING wa Mwana FA na BREAK IT DOWN wa Lil Bebbie zenye Picha za wanawake wakiwa nusu uchi katika muda ambao idadi kubwa ya watazamaji ni watoto.

wanaotutazama


hit counter

tz shiling exchange

MY CALENDAR

Total Pageviews

Recent Posts

find us on twitter

Find Us On Facebook

MATANGAZO