Saturday, 6 August 2016



Serikali chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto imepokea msaada wa shilingi bilioni 142.23 kutoka nchi washiriki Canada, Denmark, Uswizi na Korea Kusini ili kusaidia kuinua vituo vya afya nchini.
Akizungumza mara baada ya kusaini msaada huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa msaada huo wataupeleka moja kwa moja katika Zahanati za vijiji,Hospitali za Wilaya na mkoa ikiwa pamoja na vituo vya afya nchi nzima.
“Tumepokea msaada huo kwa furaha kubwa na kuhaidi kupeleka fedha hizo hizo mahali panapohitajika kwa matumizi ya kukuza na kuboresha vituo vya afya katika zahanati na hospitali nchi nzima ili kuokoa maisha ya watanzania” alisema Dkt. Ulisubisya.
Aidha Dkt. Ulisubisya anaishukuru Benki ya Dunia kwa kuimarisha na kusaidia mfuko wa maendeleo ya afya nchini kwa kuwakutanisha na wahisani kutoka nchi mbalimbali.
Mbali na hayo Dkt.Ulisubisya amewaomba Benki ya Dunia na nchi wahisani wasichoke na kushindwa kuisaidia Tanzania katika sekta ya Afya ili kutokomeza maradhi kwa kiwango kikubwa na kupambana kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi.

 















kama umependezwa na sisi jiunge nasi kwa bofya hapa ku-install application yetu Masindenews ili usisumbuke kuingia kwenye website yetu

0 comments:

Post a Comment

wanaotutazama


hit counter

tz shiling exchange

MY CALENDAR

Total Pageviews

Recent Posts

find us on twitter

Find Us On Facebook

MATANGAZO