Mwigulu Nchemba Nimefanya ukaguzi wa eneo la mpaka kati yetu na nchi ya zambia kupitia mji wa Tunduma,mbali na changamoto za msongamano wa watu kwenye eneo la mpaka.Vilevile kuna tatizo la kudumu la biashara halamu ya upitishwaji wa madawa ya kulevya katika mpaka huu kwa njia ya magari.Wanaojihusisha na biashara hii waache mara moja,tumedhamiria kuikomesha na tayari tupo kazini kuhakikisha tunatokomeza hii biashara haramu.
Pia nimefanya mazungumzo na askari wa jeshi letu la polisi,uhamiaji na magereza wa mkoa wa mbeya.Wakati serikali ikipambana kuboresha maslahi na mazingira ya kazi ya kila mtumishi,jeshi kwa idara zote tunaunganisha nguvu kuhakikisha usalama na amani ya nchi yetu inakuwa ndio kipaumbele chetu cha kila siku.
"Usalama wetu,jukumu letu sote"


0 comments:
Post a Comment