Huku Burundi akiendelea kukabiliwa
na ghasia kutoka wa upinzani baada ya kuchaguliwa kuhudumu madarakani
kwa mhula wa tatu katika mazingira yenye utata, rais wa Burundi Pierre
Nkurunziza ametoa ilani ya mwisho kwa wale aliowataja kuwa watenda
mabaya kujisalimisha.
Haya yanajiri wakati mauaji yakiendelea kuripotiwa katika mji mkuu wa Bujumbura.Nkurunziza, amewataka wapinzani kukomesha vurumai nchini humo.
Anasema kuwa sheria mpya ya kukabiliana na ugaidi, itaanzishwa ifikiapo mwisho wa mwezi huu wa Novemba.
Watu kadhaa wameuwawa na milipuko imekuwa ikisikika kila kuchao, hasa mjini Bujumbura, tangu mwezi Aprili, pale rais alipotangaza azma ya kuwania muhula wa tatu.
Nkurunziza ametoa agizo wajiepusha na uhasama.
Vyombo vya habari visivyo vya kiserikali vimefungwa huku shirika ya kupigania haki za kinadamu zikilazimika kuondoa wafanyikazi wao nchini humo kwa hofu ya kukabiliwa na vyombo vya dola.

0 comments:
Post a Comment