Tuesday, 3 November 2015



Zaidi ya wafanyakazi 50 wa shirika la umeme nchini, Tanesco mkoani Mbeya wamenusurika kifo baada ya vyuma vizito ambavyo vimetumika kutengenezea jukwaa la ujenzi wa jengo lenye urefu wa ghorofa 11 mali ya mfuko wa taifa ya bima ya afya kuporomoka na kufunika ofisi za Tanesco makao makuu ya mkoa wa Mbeya. hilo limetokea majira ya saa saba mchana baada ya mvua kubwa ya mawe ambayo imeambatana na upepo mkali kunyensha na kusababisha vyuma hivyo kuporomoka na kuangukia jengo la Tanesco hali ambayo imesababisha wafanyakazi wa shirika hilo kupatwa na hofu kiasi cha kuondolewa haraka ndani ya jengo hilo kama ambavyo meneja wa Tanesco mkoa wa Mbeya anavyoelezea.
Meneja huyo wa Tanesco mkoa wa Mbeya amesema tukio hilo limesababisha hasara kubwa kwa kampuni, ikiwa ni pamoja na uharibufu wa jengo na watumishi kushindwa kufanya kazi.baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco wamesema kuwa tukio hilo ambalo limetokea wakiwa kazini ndani ya jengo hilo limewasababishia mshtuko mkubwa huku wakidai kuwa tangu kuanza kwa ujenzi huo kumekuwepo na matukio yanayo hatarisha maisha yao kutokana na wakandarasi wanaojenga jengo hilo kutokuwa makini.

0 comments:

Post a Comment

wanaotutazama


hit counter

tz shiling exchange

MY CALENDAR

Total Pageviews

Recent Posts

find us on twitter

Find Us On Facebook

MATANGAZO