Mwanajeshi wa Israel amemuua raia
wa Israel Myahudi kimakosa baada ya wawili hao kukabiliana kila mmoja
akidhani mwenzake alikuwa Mwarabu aliyepanga kushambulia, ripoti
zinasema.
Mwanamume huyo amepigwa risasi baada yake kujaribu kutwaa bunduki ya mwanajeshi huyo kwenye mfarakano.Kwa mujibu wa ripoti kwenye vyombo vya habari nchini Israel, mwanamume huyo Mwisraeli aliwakabili wanajeshi wawili wa Israel waliokuwa wakiabiri basi katikati mwa Jerusalem Alhamisi, akidhani walikuwa washambuliaji.
Polisi wanasema wanajeshi hao nao walimshuku mwanamume huyo kuwa mshambuliaji na wakamwitisha kitambulisho chake. Alikataa kutoa kitambulisho na mfarakano ukazuka. Ni hapo ambapo mwanamume huyo alishika bunduki ya mwanajeshi moja lakini akapigwa risasi na kuuawa na mwanajeshi huyo mwingine.
Kisa hicho kimetokea huku wasiwasi ukizidi kupanda kutokana na ongezeko la mashambulio dhidi ya Waisraeli na pia uhasama kati ya Waisraeli na Wapalestina.
Alhamisi, Wapalestina wawili walipigwa risasi baada ya kumdunga kisu na kumjeruhi Mwisraeli katikati mwa Israel, polisi wanasema.

0 comments:
Post a Comment