Monday, 14 December 2015
10:01
Unknown
No comments
Lema atangazwa Mshindi
Msimamizi huyo wa Uchaguzi katika Jimbo la Arusha, amemtangaza Mbunge Mteule wa Jimbo hilo kuwa ni Godbless Lema aliyeshinda kwa kura, 68,848 sawa na 65.9%, akifuatiwa kwa mbali na Philemon Mollel (CCM) kwa kura 35,907 sawa na 34.4% kati ya wapiga kura walioandikishwa 317,814 ambapo waliopiga kura walikuwa 105,800 sawa na 32.83% huku kura halali zikiwa 104,353 na kura zilizoharibika ni 1447.
Jimbo la Handeni Mjini
Wakati huo huo, wagombea watano kutoka vyama vya ADC, CCM, CHADEMA, CUF na TLP, wamesimama kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Handeni Mjini mkoani Tanga kufuatia kifo cha aliyekuwa mgombea wa Jimbo hilo marehemu Dk. Abdallah Kigoda, kilichotokea siku chache kabla ya uchaguzi Oktoba 25, 2015.
Katika Jimbo hilo, wapiga kura 38, 597 walijiandikisha kupiga kura katika vituo 114, ambapo pamoja na idadi kubwa hiyo ya waliojiandikisha bado mwitikio sio mzuri katika uchaguzi huo.
Msimamizi wa Kituo cha Shule ya Msingi, Kwenjugo namba moja, Othumani Twalibu, amezungumzia baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na daftari la wapiga kura kutokuwa na picha za wahusika.
CCM yaibuka mshindi Handeni
Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo mdogo katika jimbo hilo, Tweneth Haule, amesema idadi ya wagipga kura ilikuwa ndogo.
Msimamizi huyo wa uchaguzi amemtangaza, Omari Abdallah (CCM) kuwa mshindi wa uchaguzi huo kwa kupata kura 10,315 akifuatiwa kwa mbali na mgombea wa Chadema, Daudi kilo Lusewa, aliyepata kura 648. Idadi ya waliojiandikisha kupiga kura ni 38,610 na idadi ya waliopiga kura 13,805 huku kura halali zikiwa ni 13,591 wakati zilizotaliwa ni 214.
Majimbo Saba yaliyokuwa hayajafanya uchaguzi Oktoba mwaka huu
Kumbukumbu zinaonyesha kwamba, hadi sasa jumla ya majimbo matano yamekwishafanya uchaguzi kati ya majimbo saba ya Tanzania Bara na moja la Zanzibar ambayo hayakufanya uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali 25 October 2015.
Miongoni mwa majimbo hayo ni pamoja na lile la Lulindi lililopo mkoani Mtwara, ambapo Chama cha ACT Wazalendo kilipata kura 213, CCM 17715, CUF 714, NLD 1638 (CHADEMA haikusimamisha mgombea). Matokeo katika Jimbo la Lushoto mkoani Tanga yanaonyesha kuwa Chama cha ACT Wazalendo kilipata kura 375, CCM 19775, CHADEMA 4402 na CUF 350.
Aidha, Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro Chama Cha ACT Wazalendo kilipata kura 626, CCM 25902, CHADEMA 10592. Matokeo ya chaguzi hizo ndogo katika Jimbo la Handeni Mjini yanaonyesha kuwa Chama Cha ACT Wazalendo kilipata kura 194, CCM 12698, CHADEMA, 632, CUF 2522 na TLP 13.
Jimbo la Arusha mjini, Chama Cha ACT Wazalendo kilipata kura 359, CCM 34849, CHADEMA 67250 na CUF 96, Katika Majimbo hayo matano, CCM imeshinda majimbo manne na CHADEMA wamepata jimbo moja. Majimbo ya Masasi na Ludewa mkoani Njombe, yanategemewa kufanya uchaguzi wake Jumapili ya 20 December 2015. chanzo FikraPevu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 comments:
Post a Comment