Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya
Kimbari ya Rwanda (ICTR) imeamua waziri mmoja wa zamani wa Rwanda
atumikie kifungo cha miaka 47 jela kwa mchango wake mauaji ya kimbari ya
1994.
Pauline Nyiramasuhuko ni mmoja wa washtakiwa sita waliokuwa
wamekata rufaa kwenye mahakama hiyo maalum ambayo imemaliza kazi yake.Alikuwa amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani awali, lakini mahakama ikaamua kupunguza adhabu dhidi yake, sawa na adhabu dhidi ya Arsène Shaim Ntahobali na Elie Ndayambaje.
Kesi hizo zilikuwa za mwisho kusikizwa na mahakama hiyo kabla ya kufungwa rasmi baada ya kusikiza kesi dhidi ya washukiwa wa mauaji hayo kutoka mjini Arusha, Tanzania kwa miaka 21. chanzo bbc


0 comments:
Post a Comment