Friday, 27 November 2015

 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjVIZ0Re-1Pktuo2kK07CN0QhGqHMK4WC5f678FUguFOjTq7Ez4xp-bs8_cRHaC0475gFqPyVFH_ZALuAkQr9sbQVHH1jBgUf3jVESLkLoEIsoJ97BVNmOQDu6srdqTJa6JTPjf875XxwLy/s1600/DSC_1787.JPG
Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta uozo . Maafisa hao wametakiwa kusalimisha hati zao za kusafiria, nah ii imekuja baada ya kugundulika kuwa kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo data za Mamlaka ya Bandari inazo lakini katika mtandao wa TRA hayaonekani.

aidha Maafisa wengine waliosimamishwa kazi ni Mkuu wa kitengo cha TEHAMA, Bw. Haruni Mpande, Bw. Hamisi Ali Omari (hakutaja ni wa idara gani), na Mkuu wa Kitengo cha Bandari Kavu (ICD In-Charge), Bw. Eliachi Mrema. “Hawa wanasimamishwa kazi hadi uchunguzi utakapokamilika na pia wawe mikononi mwa polisi,” alisema.
Pia aliagiza watumishi watatu wa mamlaka hiyo wahamishwe kutoka Dar es Salaam na kupelekwa mikoani. Watumishi hao ni Bw. Anangisye Mtafya, Bw. Nsajigwa Mwandengele na Bw. Robert Nyoni.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEirg29j0sqcdBUw3jGm2ewkX_N2DIrcWk9euDiUmNEf2BUn7JPgVX6NBxOOOKKmMcdz67tPWHER0GbTjVuIizhIIJf4voIdydx2iMGvkfMLsK4akt0yQou09Wu2ATR8XBm4fC0w51Rx1ZZD/s1600/DSC_1813.JPG
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemwagiza Katibu Mkuu wa Hazina, Dk. Servacius Likwelile ambaye alikuwepo kwenye kikao hicho, kuhakikisha kuwa anapeleka wataalamu kutoka Wakala wa Serikali Mtandao (e-Govt) haraka iwezekanavyo ili wakakague mifumo ya taarifa na kubaini jinsi ambavyo wizi huo unafanyika.
“Ninataka uchunguzi uanze kufanyika mara moja, tafuteni njia ambazo zinatumika kama mianya ya wizi kutokea hapa bandarini hadi kwenye ICDs. Nataka hayo makontena yatafutwe hadi yajulikane yako wapi, na fedha hiyo ihakikishwe inarudi serikalini,” alisema.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Bw. Ernest Mangu, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Suleiman Kova, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Bw. Awadh Massawe na viongozi mbalimbali kutoka TRA na TPA.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjI3fxqU515GGJdrIVAT2mvqeBDXPqrImRcNXYlX6CHe4Vqwzo5OJ2SlgrrLV7IaN9gbauzSky9chSi5OzzBFx0hhmLJndpboVx3CZZFLShYcLiZVotB9ROXQcB5ERPB6r7PHjOed8xRd47/s1600/45.jpg
aidha Rais John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi kamishna wa mamlaka ya mapato TRA Bw.Rished Bade na kumteua Bw.Philiph Mpango kukaimu nafasi hiyo. Aidha rais Magufuli amemtaka Rished Bade kutoa ushirikiano kwa Philiph Mpango wakati uchunguzi ukiendelea.

0 comments:

Post a Comment

wanaotutazama


hit counter

tz shiling exchange

MY CALENDAR

Total Pageviews

Recent Posts

find us on twitter

Find Us On Facebook

MATANGAZO