Thursday, 26 November 2015

Magufuli

Taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue imesema afisa yeyote wa serikali anayepanga kuchapisha au kutengeneza kadi kama hizo anafaa kufanya hivyo "kwa gharama zake mwenyewe”.
Hatua hiyo inaonekana kuwa ya karibuni zaidi kwa serikali kubana matumizi tangu kuingia madarakani kwa Rais John Pombe Magufuli mapema mwezi huu.
"Fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji na uchapishaji wa kadi, zitumike kupunguza madeni ambayo Wizara, Idara na Taasisi za umma zinadaiwa na wananch/wazabuni waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe katika matumizi mengine ya kipaumbele,” imesema taarifa iliyotoka kwa kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ya Ikulu Bw Gerson Msigwa.Miongoni mwa hatua alizochukua Rais Magufuli ni kubana safari za nje za maafisa wa serikali, kupunguza matumizi ya pesa sherehe ya wabunge na kuagiza zitumie hospitali ya taifa ya Muhimbili na pia kufuta sherehe za Siku ya Uhuru mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment

wanaotutazama


hit counter

tz shiling exchange

MY CALENDAR

Total Pageviews

Recent Posts

find us on twitter

Find Us On Facebook

MATANGAZO