Friday, 6 November 2015



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika wizara ya fedha kwa kutembea kwa miguu kutoka ofisini kwake Ikulu hadi wizarani hapo na kuwataka watendaji wakuu wa wizara hiyo kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwa kukusanya kodi hasa kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa ambao wanadaiwa kukwepa kodi ili serikali iweze kutoa huduma za kijamii kwa wananchi hasawa hali ya chini ikiwemo kutoa elimu bure kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kuanzia mwakani.
Mapema asubuhi kabla ya kufanya tukio hilo linaloelezwa si la kawaida na la kushtukiza rais Dr John Pombe Magufuli ameanza siku yake ya 
kwanza ofisini kwa kumuapisha mwanasheria mkuu wa serikali George Masaju akizungumzana vyombo vya habari mara baada ya kuapishwa mwanasheria mkuu huyo wa serikali amesema ofisi yake imekuwa ikijitahidi kukabiliana na changamoto kadha wa kadha ikiwemo kesi za jinai na madai zinazofunguliwa dhidi ya serikali ambapo ofisi hiyo imefanikiwa kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kwa kushinda baadhi ya kesi hizo.
Pia rais Dr John Pombe Magufuli mara baada ya tukio hilo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa kimataifa Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo amekutana na makamu mwenyekiti wa chama cha tawala cha China Zhang Ping, kisha waziri wa kazi wa Angola Joaobabtista, halafu waziri wa nchi wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Algeria Ramtane Lamamra, spika wa bunge la Burundi Pascal Nyabenda na kumalizia na waziri wa kilimo wa Misri Essam Fayed.
Pia rais Dr Magufuli pamoja na wafanyakazi wa Ikulu wakapata fursa ya kumuaga rais mstaafu Dr Jakaya Mrisho Kikwete aliyeambatana na 
familia yake yote na kuwataka watumishi hao kutoa ushirikiano wa kutosha kwa rais mpya kabla hajakwea helkopta na kuondoka katika eneo la ikulu. chanzo itv

0 comments:

Post a Comment

wanaotutazama


hit counter

tz shiling exchange

MY CALENDAR

Total Pageviews

Recent Posts

find us on twitter

Find Us On Facebook

MATANGAZO