Washukiwa wawili wamefariki baada ya
maafisa wa usalama kushambulia Saint Denis kaskazini mwa Paris,
wakisaka waliohusika mashambulio ya Ijumaa.
Ufyatulianaji mkali wa
risasi umetokea mapema asubuhi kwenye mtaa huo. Operesheni hiyo
inadaiwa kumlenga mwanamgambo wa Islamic State Abdelhamid Abaaoud ambaye
amedaiwa kupanga mashambulio hayo yaliyoua watu 129.Maafisa kadha wa polisi wamejeruhiwa kwenye operesheni hiyo, kituo cha runinga cha BFMTV cha Ufaransa kimeripoti.
Video iliyoonyeshwa na vituo vya televisheni vya BFMTV na iTele zimeonyesha watu walioshuhudia wakisema milio ya risasi ilianza kusikika saa kumi unusu alfajiri saa za Ufaransa.
Naibu meya Stephane Peu amewahimiza raia wasalie manyumbani, akisema "hili si shambulio jipya bali ni operesheni ya polisi".chanzo bbc

0 comments:
Post a Comment