Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
ameagiza kukamatwa kwa afisa mmoja mkuu serikalini kwa tuhuma za kuiba
zaidi ya dola bilioni 2 zilizotengewa vita dhidi ya kundi la Boko Haram.
Kanali
Sambo Dasuki ambaye alikuwa mshauri wa kitaifa kuhusu maswala ya
usalama kwa aliyekuwa rais Goodluck Jonathan ,ameshtakiwa kwa kutoa
kandarasi bandia za kununua helikopta 12,ndege 4 za kijeshi na silaha.Lakini vifaa hivyo havijawasili na mshauri huyo wa zamani anadaiwa kuiba fedha hizo.Tayari amekana madai hayo.
Msemaji wa rais Buhari ameiambia BBC kwamba ufisadi huo ulisababisha vifo vya maelfu ya raia wa Nigeria.
Wanajeshi wa taifa hilo wamelalamika kwamba licha ya kiasi kikubwa cha fedha kinachotumiwa kununua vifaa vya kijeshi hawana vifaa vya kuweza kukabiliana na kundi la Boko haram.chanzo bbc

0 comments:
Post a Comment