Viongozi wa mataifa 20 yenye uchumi
mkubwa zaidi duniani wanakutana huko Uturuki ambako ajenda ya vipi
kukabiliana na vitendo vya ugaidi vinatarajiwa kutawala mazungumzo yao.
Mengi ya mataifa yanayoshiriki kikao hicho yamewahi kukumbwa na mashambulio kama hayo.Rais wa Uturuki Tayip Erdogan, anatarajiwa pia kuhimiza hatua za kumaliza vita vya Syria.
Rais wa Marekani Barrack Obama amesema kuwa wanaandaa mikakati ya kujibu mashambaulizi ya alyopangwa na Islamic State mjini Paris Ufaransa.
Duru za White House zasema rais Obama anatarajiwa kuwa na kikao na mfalme wa Salman wa Saudia hapo kesho kama njia mojawapo ya kutafuta suluhu kwa mzozo wa Syria.
Wakati huohuo mashirika 20 na mataifa yakiwemo Urusi na Marekani wanasema - makubaliano yameafikiwa ya ratiba iliyopangwa kujaribu kumaliza vita vya Syria.
Mpango huo uliafikiwa baada ya mkutano mjini Vienna Austria
Hata hivyo bado hamna mwafaka mahsusi kuhusu mstakabali wa baadaye wa rais , Bashar al-Assad.
chanzo bbc


0 comments:
Post a Comment