Hatimaye kamati kuu ya chama cha mapinduzi CCM imetegua kitendawili cha majina ya makada watatu watakaowania kuchaguliwa kugombea nafasi ya uspika wa bunge la 11 kupitia chama hicho kwa kuwatangaza naibu mwanasheria mkuu wa Tanzania Dk Tulia Atson, Mbunge wa Afrika Mashariki Abdula Mwinyi na naibu spika wa bunge la 10 Job Ndugai kuwa wagombea.
Katibu wa NEC itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye anataja majina
hayo baada ya kukamilika kwa kikao cha kamati kuu kilichokutana
takribani saa moja na nusu kikitanguliwa na kikao cha kamati ya maadili
kupitia majina ya makada 21 waliojitokeza kuomba nafasi hiyo.chanzo


0 comments:
Post a Comment