Tuesday, 10 November 2015


Mwanahabari mashuhuri nchini Kenya anazuiliwa na maafisa wa usalama Kenya baada ya kudaiwa kuchapisha habari kuhusu tuhuma za ufisadi serikalini.
Mwanahabari huyo John Ngirachu wa shirika la habari la Nation Media Group anadaiwa kuandika taarifa iliyonukuu habari kutoka kwa kikao cha faraghani cha Kamati ya Bunge kwenye gazeti la Daily Nation.
Habari hizo zinahusu ufisadi katika Wizara ya Usalama na Masuala ya Ndani kuhusu matumizi ya Sh3.5 bilioni pesa za Kenya.
Waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery,anasema aliwasilisha habari hizo faraghani na anasema yeyote aliyefichua habari hizo sharti aeleze alizitoa wapi.
“Kama waziri anayesimamia usalama, nachukulia hatua hii kama njama ya kudhuru taifa, kuhujumu juhudi za kudumisha usalama na kuonyesha wizara hii kama fisadi na isiyofuata sheria.
"Haikubaliki,” alisema Nkaiserry kwenye kikao na wanahabari siku moja baada ya kuchapishwa kwa habari hizo.
Lakini mmoja wa wahariri wakuu wa shirika la habari la Nation Media, Linus Kaikai amekanusha madai hayo
“Hatujakiuka maadili yoyote, vikao vya bungeni wazi na katika katiba tunaruhusiwa kuwa katika vikao vile’’.
"Habari hizo zilijulikana Nkasissery alipofika katika kikao hicho cha kamati ya bunge,” Bw Linus Kaikai ameiambia BBC.
“Kwa sasa mawakili wetu wanashughulika kujaribu kumtoa korokoroni’’.
‘’Kwa sasa kile tunajali zaidi ni uhuru wa Ngirachu.”chanzo bbc

0 comments:

Post a Comment

wanaotutazama


hit counter

tz shiling exchange

MY CALENDAR

Total Pageviews

Recent Posts

find us on twitter

Find Us On Facebook

MATANGAZO