Polisi wa Texas wamemuondolea mashtaka mvulana mwislamu mwenye umri wa miaka 14 aliyekamatwa kwa kutengeza saa.
Maafisa
katika shule ya upili ya Mac Arthur mjini Irving waliwaita maafisa wa
polisi baada ya kudhania kwamba saa hio ilikuwa bomu.
Kukamatwa kwa Ahmed Mohammed kumekosolewa na wengi huku kijana huyo akipata mwaliko katika ikulu ya White House nchini Marekani.
Katika mkutano huohuo na vyombo vya habari,Ahmed amesema kuwa anataka kuihama shule hiyo.
''Ni
kijana mwerevu sana na kwamba alisema anataka ulimwengu umjue''.Mafisa
wa polisi hatahivyo wamekana madai ya familia ya Ahmed kwamba alikamatwa
kutokana na jina lake.
''Tumekuwa na uhusiano mzuri na jamii ya
waislamu'', alisema mkuu wa polisi wa eneo la Irving Larry Boyd siku ya
jumatano.''Visa kama hivi hutoa changamoto.Tunataka kukichukulia kisa
hiki kama funzo zuri''.chanzo bbc


0 comments:
Post a Comment