Mapambano yamezuka kwenye hoteli
katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, ambako mazungumzo ya amani
yamekuwa yakifanyika, baada ya mapinduzi ya juma lilopita.
Wafuasi
kama 50 wa kikosi cha kumlinda rais, ambacho kiliipindua serikali ya
mpito Alhamisi, kiliingia kwa nguvu katika ukumbi wa hoteli, na kujeruhi
waandishi wa habari kadhaa.Watu kama 10 wameuwawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa katika mapambano baina ya wanajeshi na waandamanaji katika siku chache zilizopita.
Mazungumzo yamekuwa yakifanyika katika mji mkuu Ouagadougou baada ya siku ya tatu ya maandamano ya kupinga mapinduzi ya rais Kafando yaliyofanywa na kikosi cha kumlinda rais.
Haijabainika hadi kufikia sasa kiongozi wa mapinduzi haya atatoa masharti yepi ya kurejesha mamlaka kwa rais Kafondo na utawala wake.chanzo bbc

0 comments:
Post a Comment