Shirika linalosimamia safari za
ndege nchini Kenya, KCAA, limetangaza kuwa anga ya Kenya itafungwa kwa
muda wa dakika hamsini siku ya Ijumaa wiki hii ili kuruhusu ndege ya
rais wa Marekani Barrack Obama kutua katika uwanja wa kimataifa wa ndege
wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.
Kwa mujibu wa shirika hilo, agizo
hilo litatekelezwa katika viwanja vyote vya ndege nchini Kenya na kuwa
anga hiyo itafunguliwa muda tu pale ndege hiyo ya rais Obama itakapokuwa
imetua.Shirika hilo limesema kuwa limeyaandikia mashirika yote ya ndege na pia kampuni zote za usafiri kuhusiana na agizo hilo na kuwa safari za ndege kadhaa zitacheleweshwa siku hiyo na pia siku ya jumapili wakati rais Obama atakapokuwa akiondoka nchini Kenya kuelekea Ethiopia kwa muda wa dakika arubaini.


0 comments:
Post a Comment