Thursday, 16 July 2015

Viongozi wawili wa kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Al shabaab nchini Somalia wameuawa kwenye shambulio la mabomu ya angani.
Watu katika mji wa Baardhere ulioko kusini mwa nchi hiyo wanasema walisikia milipuko asubuhi ya leo katika eneo hilo.
Kisha wapiganaji hao wa Al shabaab wakafika eneo hilo la tukio.
Baardheere ni moja ya miji ambayo bado ingali inadhibitiwa na wapiganaji wa Al shabaab.
Wanajeshi wa muungano wa Afrika na wale wa serikali ya Somalia wanakaribia eneo hilo.
Viongozi kadhaa wa kundi hilo wameuawa kwenye mashambulio ya mabomu ya angani yaliyoangushwa na wanajeshi wa Marekani. bbc

0 comments:

Post a Comment

wanaotutazama


hit counter

tz shiling exchange

MY CALENDAR

Total Pageviews

Recent Posts

find us on twitter

Find Us On Facebook

MATANGAZO