Wiki hii maskio yote ya
Watanzania yanaelekezwa mjini Dodoma, mji mkuu wa Tanzania ambapo chama
tawala nchini humo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinamchagua mtu mmoja
atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa wabunge
na rais unaotarajiwa kufanyika tarehe 25 Oktoba 2015.
Vikao
vya mchakato huo vinaanza rasmi Jumatano huku vikitanguliwa na kikao
cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ambayo kimsingi pamoja na mambo mengine
kitapitia wasifu wa watia nia wote lakini pasipo kupunguza jina lolote.Siku ya Alhamisi (09 Julai), Kamati Kuu ya chama yenye wanachama takribani 32 itakutana na hapo ndipo upungazaji wa majina utafanyika hadi kufikia majina matano tu.
Baada ya hapo, Halmashauri kuu ya chama itakutana siku ya Ijumaa tarehe 10 Julai ambapo itachuja majina hayo matano hadi kufikia matatu kupitia mtindo wa kupiga kura. Majina haya matatu ndiyo yatakayokwenda katika Mkutano Mkuu wa Chama ambao ndio utakaochagua jina moja la huyo mgombea urais kwa tiketi ya chama
Mkutano Mkuu huu unajumisha takribani wanachama 2100 ikiwa ni pamoja na Wabunge wa CCM Tanzania bara na wawakilishi wengine kutoka Zanzibar lakini pia wawakilishi wa chama kutoka ngazi mbalimbali hadi zile za chini.
CHANZO BBC


0 comments:
Post a Comment