Sunday, 6 December 2015


Uongozi wa shirika la umeme nchini Tanesco umewafukuza kazi wafanyakazi saba waandamizi wa shirika hilo wakiwemo mameneja kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo vitendo vya wizi, kudai rushwa, ubadhirifu wa mali wa shirika hilo pamoja na kutoa lugha chafu kwa wananchi jambo ambalo ni kinyume na taratibu za maadili ya kazi na uongozi huo kuwaonya wafanyakazi wengine wenye tabia kama hizo kwamba watachukuliwa hatua.
Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Mhandisi Felichesm Mramba akitoa taarifa juu ya uumuzi wa kufukuzwa kazi kwa wafanyakazi hao saba kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema uamuzi huo umechukuliwa ikiwa ni mpango endelevu wa shirika la Tanesco kuimrisha nidhamu kwa wafanyakazi wake kutambua wajibu wao wa kutoa huduma ya nishati kwa wananchi na sio na sio kuwasumbua wateja na kutaja vitengo ambavyo wafanyakazi hao wamefukuzwa ikiwemo ngazi ya mameneja, wahandisi na wahasibu kutoka mikoa ya Kinondini kaskazini, Katavi, Kagera na Ilala.

0 comments:

Post a Comment

wanaotutazama


hit counter

tz shiling exchange

MY CALENDAR

Total Pageviews

Recent Posts

find us on twitter

Find Us On Facebook

MATANGAZO