Wednesday, 16 December 2015


Waziri wa Kilimo,Uvuvi na Ufugaji Mhe. Mwigulu Nchemba atembelea majerui wa mgogoro uliotokea katika kijiji cha Dihinda wilayani Mvomero mkoani Morogoro. Waziri Nchemba amechukua hatua ikiwemo kuunda kamati za usuluhishi wa migogoro kwa kila kijiji zitakazohusisha pande zote mbili ili kubaini wavamizi wa maeneo na kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika na tukio hilo.

 
"ANatoa rai kwa Wananchi hususani wa jamii ya Wafugaji na Wakulima,Hakuna ardhi au Mnyama mwenye thamani sawa na Maisha ya Mwanadamu yeyote yule,njia bora na salama ya kutatua migogoro hii inayohusisha wakuliama na wafugaji ni kufuata taratibu za kuonana na Uongozi wa serikali wa eneo husika hatua kwa hatua,Nawaomba wananchi waache kujichukulia sheria mikononi.Tunakwenda kuunda kamati za usuruhishi wa migogoro hii kwa kila kijiji zitakazohusisha pande zote mbili ili kubaini wavamizi wa maeneo na kuwachukulia hatua za kisheria."
Nimeagiza kupitia kwa Mkuu wa wilaya na kamati yake ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Mvomero(kwa husika maeno yote ya Nchi yetu) kuhakikisha wanaimarisha ulinzi maeneo yote yenye migogoro,pili wahakikishe waliosababisha maafa wanakamatwa mara moja na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia.
Kwa walio jeruhiwa,nimeagiza wapatiwe matibabu kwanza bila kuchelewa na hatua za kisheria kwa wenye hatia zifuate.









0 comments:

Post a Comment

wanaotutazama


hit counter

tz shiling exchange

MY CALENDAR

Total Pageviews

Recent Posts

find us on twitter

Find Us On Facebook

MATANGAZO