Wednesday, 21 October 2015

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema demokrasia ya kweli ni kukubali ukweli, hivyo wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumapili, wanapaswa kujiandaa kisaikolojia kukubali matokeo pindi watakaposhindwa.
Amesema siku chache zijazo atabadilika na kuitwa Waziri Mkuu mstaafu, hivyo amejiandaa kisaikolojia kuondoka ofisini na hivyo watakaoshindwa Uchaguzi Mkuu wakubali ukweli huo ili nchi iendelee kubaki na amani.
Pinda aliyasema hayo jana, Dar es Salaam akiwa mgeni rasmi katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa Victoria Place wa ujenzi wa jengo la makazi na biashara unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Alisema katika nchi yoyote yenye demokrasia, watu wake wanapaswa kutambua kwamba katika purukushani za mashindano kuna mshindi na mshindwa ingawa ukweli halisi wa demokrasia unatambua hata aliyeshindwa kuwa ni sehemu ya mshindi.
“Tujiandae kisaikolojia. Demokrasia ni kukubali ukweli,” alisema Pinda akieleza wazi kuwa anatumia nafasi hiyo kusema hayo kama sehemu ya kuaga kwa kuwa hadhani kama atapata jukwaa jingine la NHC kuyasema hayo akiwa Waziri Mkuu.
Aliwataka Watanzania wenye sifa za kupiga kura, kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao kuchagua viongozi watakaolipeleka taifa mbele na aliwataka wakimaliza kupiga kura, warejee nyumbani kupumzika na kusubiri matokeo.
“Tupo katika kipindi cha lala salama, kuna watu wanasema ovyo, mara mlinde kura, kura zinalindwa na mawakala hivyo lazima vyama vihakikishe vina mawakala waaminifu,” alisisitiza Pinda.
Pinda aliwakumbusha Watanzania kuendelea kumsihi Mungu ili uchaguzi uwe wa amani na kuwakumbusha watumishi wa umma na Watanzania kutambua kuna maisha baada ya Uchaguzi Mkuu.chanzo habari leo

0 comments:

Post a Comment

wanaotutazama


hit counter

tz shiling exchange

MY CALENDAR

Total Pageviews

Recent Posts

find us on twitter

Find Us On Facebook

MATANGAZO