Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt
Abdallah Kigoda alifariki dunia siku ya Jumatatu nchini India alipokuwa
amelazwa akipatiwa matibabu.
Katibu wa Bunge la Tanzania Dkt
Thomas Kashilila amethibitisha taarifa hizo, na kusema kuwa Dkt Kigoda
alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Apollo, New Delhi nchini IndiaKitengo cha Habari na Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge, kimesema taarifa zaidi kuhusu msiba na taratibu za kurejesha mwili nchini Tanzania zitaendelea kutolewa na Serikali na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu kadiri zinavyoendelea kupatikana. chanzo bbc

0 comments:
Post a Comment