Licha ya mwenyekiti wa tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kutangaza kufutilia mbali kwa
matokeo ya uchaguzi visiwani humo akisema uchaguzi huo ulijaa kasoro
nyingi,
Tume ya uchaguzi Tanzania NEC imetoa ilani kuwa hatua hiyo
haitaathiri kwa njia yeyote matokeo ya uchaguzi wa urais Tanzania
bara.Kupitia kwa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari mwenyekiti wa NEC jaji mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa
''Uvumi unaoendelea kwamba, Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa umefutwa siyo kweli, ni uvumi, uongo, ni upotoshwaji.''
''Hadi sasa Tume imeshapokea matokeo ya kura za Rais kutoka majimbo yote ya Zanzibar na imeshayatangaza.''
Jaji Lubuva anaendelea kusema kuwa,
''Uchaguzi wa rais na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaosimamiwa na tume ya taifa ya uchaguzi ni tofauti na Uchaguzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.'
Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi kisiwani Zanzibar (ZEC) Salim Jecha alifutilia mbali matokeo akisema kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki.
Jecha aliwatuhumu baadhi ya makamishna wa tume yake kwa kuwa ''wawakilishi wa vyama vyao".
Tume hiyo ya uchaguzi ilikuwa imetangaza matokeo yamajimbo 31 kati ya majimbo 54 visiwani humo. chanzo bbc

0 comments:
Post a Comment