Saturday, 31 October 2015

Jamaa

Watu 224 wamefariki baada ya ndege ya shirika moja la Urusi kuanguka katika eneo la Sinai nchini Misri.
Ndege hiyo aina ya Airbus A-321 ilikuwa imetoka mji wa Sharm el-Sheikh ikielekea mji wa St Petersburg nchini Urusi ilipoanguka.
Maafisa wa serikali wa Misri wamenukuliwa na shirika la habari la AP wakisema hakuna manusura wowote waliopatikana.
Maafisa wa usalama eneo hilo wameambia shirika la habari la Reuters kwamba kufikia sasa miili 150 imepatikana.
Rais wa Urusi Vladimir Putin ametuma risala za rambirambi kwa jamaa za waathiriwa na kuagiza uchunguzi ufanywe.
Ujumbe kutoka Urusi ukiongozwa na Waziri wa Uchukuzi Maksim Sokolov umeelekea eneo la mkasa huku Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi naye akirejea nyumbani kutoka Bahrain.
Awali, kulikuwepo na utata kuhusu hatima ya ndege hiyo, baadhi ya ripoti zikisema ilitoweka karibu na visiwa vya Cyprus. Lakini afisi ya Waziri Mkuu wa Misri Sharif Ismail imethibitisha kwamba ndege hiyo ilianguka katikati mwa eneo la Sinai.
Afisi hiyo imeongeza kuwa Bw Ismail ameunda kamati ya dharura ya kushughulikia ajali hiyo.
Wengi wa abiria walio kwenye ndege hiyo ni watalii kutoka Urusi.
Ndege hiyo ni ya shirika la ndege la Kogalymavia. Ripoti za karibuni zinasema ilikuwa imewabeba abiria 217 na wahudumu saba.chanzo bbc

0 comments:

Post a Comment

wanaotutazama


hit counter

tz shiling exchange

MY CALENDAR

Total Pageviews

Recent Posts

find us on twitter

Find Us On Facebook

MATANGAZO