Monday, 12 October 2015

Wanawe Mubarak


Mahakama nchini Misri imeagiza kuachiliwa huru wa wana wawili wa kiume wa rais aliyeng’olewa mamlakani Hosni Mubarak.
Wawili hao walikuwa wamefungwa jela miaka mitatu kwa kuhusika katika ufisadi, shirika la habari linalomilikiwa na serikali Nile News limeripoti.
Mahakama iliamuru Alaa na Gamal Mubarak waachiliwe huru baada ya kuzingatia muda ambao wamekaa jela, afisa wa mahakama na wakili wao Farid al-Deeb wameambia shirika la habari la AFP.
Wawili hao walikamatwa na kuzuiliwa mwaka 2011.
Bado wanasubiri uamuzi kuhusu rufani waliyokata dhidi ya hukumu nyingine ya miaka mitatu jela kila mmoja kwa ubadhirifu wa pesa za umma.
Walikuwa pia wanatajwa katika kesi kuhusu kuingilia na kuchezea soko la hisa.chanzo bbc


0 comments:

Post a Comment

wanaotutazama


hit counter

tz shiling exchange

MY CALENDAR

Total Pageviews

Recent Posts

find us on twitter

Find Us On Facebook

MATANGAZO