Friday, 10 July 2015

Joto limepanda mjini hapa, ambapo mchujo wa kumpata mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), unaanza rasmi leo, pale Kamati Kuu (CC) itakapochuja majina ya watangaza nia 38 waliochukua na kurejesha fomu na kubakiza watano.
Kamati Kuu itachuja majina ya watangaza nia hao huku ikizingatia kile kilichochambuliwa na kupendekezwa na Kamati ya Ushauri ya CCM, inayoundwa na wazee wastaafu, iliyokutana hivi karibuni na pia Kamati ya Nidhamu na Usalama, iliyokutana kwa siku nzima jana chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.
Kamati ya Maadili na Usalama iliyokutana jana, ilihusisha wajumbe kutoka CCM na serikalini wakiwemo watendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Idara ya Usalama wa Taifa.CHANZO HABARI LEO

0 comments:

Post a Comment

wanaotutazama


hit counter

tz shiling exchange

MY CALENDAR

Total Pageviews

Recent Posts

find us on twitter

Find Us On Facebook

MATANGAZO