Thursday, 18 June 2015

Mshukiwa wa mauaji ya watu tisa katika kanisa moja la kihistoria mjini Carolina Kusini amekamatwa.
Kulingana na mwanasheria mkuu Lorreta Lynch,awali maafisa walimtaja kijana huyo wa miaka 21 kuwa Dylann Storm kama mtu waliyekuwa wakimsaka kwa shambulizi la Charleston.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa mshukiwa huyo aliyejihami na bunduki aliketi katika mkutano wa mafundisho ya biblia kwa takriban saa moja kabla ya kufyatua risasi na kuwaua wanawake sita na wanaume watatu akiwemo mchungaji wa kanisa hilo.
Maafisa wamelitaja shambulizi hilo kama la uhalifu wa chuki.
Bi Lynch
amesema idara ya haki itaangazia maswala yote ili kubaini njia mwafaka ya kumfungulia mashtaka mshukiwa.

0 comments:

Post a Comment

wanaotutazama


hit counter

tz shiling exchange

MY CALENDAR

Total Pageviews

Recent Posts

find us on twitter

Find Us On Facebook

MATANGAZO